
Marehemu
Askofu Dk. Thomas Laizer enzi za uhai wake
--
ALIYEKUWA Askofu wa
Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati,Marehemu Askofu
Dk. Thomas Laizer anatarajiwa kuzikwa Ijumaa Februari 15,
2013.
Kwa Mujibu wa Taarifa
maalum iliyotolewa na Kamati ya Mazishi ya KKKT na Familia ya Marehemu, inasema
kuwa Marehemu atazikwa katika eneo la Kanisa Kuu mjini Kati
Arusha.
Aidha taarifa hiyo
imesema kuwa waumini na Washirika wa Kanisa Kuu na makanisa yote ya KKKT nchini,
Wananchi, ndugu jamaa na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa
Mwili wa marehemu kuanzia Alhamisi Alasiri ya Februari 14,
2013.
Taarifa hiyo iliongeza
kuwa Mwili wa Askofu Laizer utalala Kanisani hapo hadi Ijumaa ya
Mazishi.
Marehemu Askofu Thomas
Laizer aliyezaliwa Machi 10, 1945 katika Kijiji cha Kitumbeni Arusha na baade
kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane Longido na kumaliza mwaka
1965.
Askofu Laizer,
aliendelea na masomo yake ya juu ndani na baade kujiunga na masomo ya Theolojia
katika chuo cha Makumira na baade kuongeza masomo nchini
Marekani.
Marehemu wakati wa uhai
wake alikuwa Mwinjilisti, Mchungaji katika makinisa mbalimbali nchini na baade
kuwa Mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Sinodi na baade kuwa Rais wa sinodi kabla ya
kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Kwanza wa Dayosisi ya Arusha ambayo kwa sasa ni
Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Marehemu Baba Askofu
Thomas Laizer ameacha mjane watoto wanne na mjukuu mmoja.
Nae Waziri Mkuu Mstaafu
Edward Ngoyai Lowasa amesema kuwa Kanisa na jamii limempoteza kiongozi na
mpigania maendeleo ya jamii kiroho na kimwili.
“Tumepoteza kiongozi wa
kiroho na kijamii,amehusika katika kuelimisha jamii kwa kuanzisha shule nyingi
za Sekondari,amehusika pia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Arusha Lutheran
Medical Center,zahanti na vituo vya afya katika vijiji kadhaa Mkoani Arusha
pamoja na hoteli ya Corridor springs”alisema Lowasa.
Aliwataka waumini wa kanisa
la KKKT kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na kiongozi
wao.
"Natoa pole nyingi kwa familia ya marehemu Baba Askofu
Laizer na kanisa la KKKT kwa ujumla wake,lakini askofu Laizer atakumbukwa kwa
utumishi uliotukuka katika siku za uhai wake"alisema Lowassa akihojiwa na kituo
cha radio cha kitaifa cha Radio one asubuhi ya jana





0 comments:
Post a Comment