Kapingaz Blog

Sunday, March 24, 2013

NCCR wapinga uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe uliopo Mbeya kupewa jina la Kikwete


 
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimepinga uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya kutaka Uwanja wa Ndege wa Songwe upewe jina la Rais Jakaya Kikwete.
NCCR pamoja na PPT Maendeleo kimependekeza kuwa uwanja huo uitwe Mbeya International Airport.
Uamuzi wa kutaka uwanja huo uitwe jina la Kikwete ulipitishwa katika kikao cha kamati hiyo kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Dk. Norman Sigalla kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
Wakizumngumza na Tanzania Daima Jumapili baada ya kikao hicho, Katibu wa NCCR-Mageuzi Wilaya ya Mbeya Mjini, George Mbojela alisema licha ya yeye kuwapo kwenye kikao hicho, alishtushwa na uamuzi huo kwani tayari kuna miradi kadhaa ya maendeleo iliyopewa jina la Rais Kikwete.
“Ni vyema wananchi wa Mbeya wangeshirikishwa kwenye kupendekeza jina la uwanja huo kwani wanaopaswa kupewa kipaumbele katika kupendekeza jina la uwanja huo ni wakazi wa Mbeya na sio wakuu wa wilaya ambao ni watu wa kupita tu,” alisema katibu huyo wa NCCR-Mageuzi.
Mwenyekiti wa PPT Maendeleo, Godfrey Devis aliungana na NCCR-Mageuzi kupinga hatua hiyo kwani inanyima fursa mkoa wao kujitangaza kimataifa.
Ujenzi wa uwanja huo wa ndege wa Songwe ulianza kwenye uongozi wa Rais Benjamin Mkapa wakati huo Profesa Mark Mwandosya akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi

0 comments: