Kapingaz Blog

Tuesday, April 23, 2013

WIZARA YA HABARI YATOA MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WAKE WAPYA LEO JIJINI DAR

 

Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 imeajiri watumishi wapya 30.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akitoa maelezo kuhusu mafunzo elekezi kwa watumishi wapya walioajiriwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13 leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Gasper Mwembezi.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Enely Mwakyoma na kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo.
Baadhi ya wakurugenzi kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza katibu mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene.
Baadhi wa waajiriwa wapya kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru (kulia) akimwambia jambo Katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Waajiriwa wapya kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakurugenzi wa Idara na Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo elekezi leo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam . Watatu kushoto mstari wa mbele ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

0 comments: