Kapingaz Blog

Thursday, May 9, 2013

MARUDIO-NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013


Coat of arms of Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alitangaza nafasi za ajira kwa Wataalam wa Kada za Afya kwa mwaka 2012/2013 ambapo tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi hayo ilikuwa tarehe 10 Mei, 2013.
Kwa tangazo hili Wananchi wanajulishwa kuwa muda wa kuwasilisha maombi hayo umeongezwa hadi tarehe 20 Mei, 2013. Aidha inasisitizwa kuwa hata wahitimu wa mwaka 2012 wanapaswa kutuma maombi yao kwa sababu hakutakuwa na utaratibu wa wahitimu kupangiwa vituo vya kazi moja kwa moja.
 
Maombi hayo yaendelee kuwasilishwa kwa njia ya Posta kwa kutumia anuani iliyopo chini ya tangazo hili.
 
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
 
KAIMU KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.

0 comments: