Kapingaz Blog

Thursday, January 12, 2017

Alichokizungumza Tundu Lissu kuhusu mbunge wa kilombero kufungwa miezi 6


HATUA ya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro kumfunga Peter Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero miezi sita jela, inatokana na visa vya kisiasa

Ni kauli ya Tundu Lissu, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo mbele ya waandishi wa habari aliokutana nao kwenye Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema kuwa, vita kati ya upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimesababisha Lijuakali (Chadema) kupata hukumu hiyo ya kisiasa.

Mbele ya waandishi wa habari Lissu amesema kuwa, “hiyo ni hukumu ya kisiasa” na kwamba, Jeshi la Polisi nalo limeingizwa kwenye vita hivyo.

Habari kwa kina bofya: HAPA

0 comments: