Kapingaz Blog

Wednesday, January 11, 2017

Anglikana Bado Ngoma Nzito........Askofu Mokiwa Atoa Utetezi Wake, Asisitiza Hatang'oka Hata Kwa Dawa


Hali  ya amani ndani ya Kanisa la Anglikana nchini, bado si nzuri baada ya Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa aliyevuliwa uaskofu kutoa msimamo wake na kudai kuwa yeye ni msafi, na ndio Askofu wa Dar es Salaam, hang’oki hata kwa dawa, na amewasamehe wanaompinga.

Askofu Mokiwa aliyasema hayo kwenye Kanisa la Anglikana Ilala jana, alipozungumza na waandishi wa habari. Alisema licha ya kusemwa mambo magumu, lakini yeye kama Askofu, kazi yake ni kuwaombea waliomkosea na hana matatizo nao, kwani amekwisha wasamehe.

Askofu Mokiwa pia alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Dayosisi ya Anglikana Dar es Salaam haina mgogoro, bali viongozi watano wa dayosisi hiyo ndio wanatengeneza mgogoro huo kwa maslahi binafsi, wakitumia Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni kama njia ya kupitishia migogoro yao.


Habari kwa kina bofya: HAPA

0 comments: