Kapingaz Blog

Friday, January 13, 2017

MKAPA, MWINYI KUONGOZA MATEMBEZI YA “WALK FOR ELPHANT DAR ES SALAAM 2017”


UYE
 Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matembezi ya kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff.Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa China House.
UYE 1
Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matembezi ya kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff.
UYE 2
 Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama akionyesha tangazo lenye ujumbe wa kuhimiza matembezi ya ku kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff. Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa China House.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
…………
Na Frank Shija-MAELEZO.
MKAPA kuongoza matembezi ya hiari ya kilomita tano yanayojulikana kama Walk for Elephant Dar es Salaam 2017yatayofanyika kesho kuanzaia saa 12 asubuhi yaikianzia Ubalozi wa China hadi Sea Cliff Hotel.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na China (TCFPA) Joseph Kahama alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na matembezi hayo leo jijini Dar es Salaam.
Kahama amesema kuwa yana lengo la kuonyesha umoja katika kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo.
“Tunatarajia kuwa na matembezi ya kwa ajili ya kupinga ujangili dhidi ya Tembo ambapo wageni wetu mashuhuri wanatarajiwa kuwa Marais wastaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mzee Mkapa atakayepokea matembezi hayo katika Hotel ya Sea Cliff,” alisema Kahama.
Aliongeza kuwa zaidi ya watu 550 wamethibitisha kushiriki katika matembezi hayo wakiwemo baadhi ya watu maarufu kama vile Jokate Mwigelo, Mrisho Mpoto na wasanii wengine.
Aidha Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na China(TCFPA) imeanzishwa kwa nia ya kudumisha urafiki na uhusiano baina ya raia wa nchini hizo mbili.
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua ni kwanin china imeamua kusaidia katika vita dhidi ya ujangili ili hali inatajwa kuwa miongoni mwa soko kubwa la bidhaa za meno ya Tembo, Kahama alisema kuwa Serikali ya China haiku tayari kuona nchi yake inatajwa kama soko la meno ya Tembo ndiyo maana Rais Xi Jinping wa China na Barrack Obama wa Marekani wamewahi kutoa tamko la pamoja la kupinga ujangili na ni kosa la jina kwa rai wa China kukamatwa na nyara hizo.
Chama hicho kimekusudia kuifanya tarehe 14 mwezi wa kwanza kila mwaka kuwa siku ya matembezi ya Walk for Elphant Dar es Salaam 2017 ili kujenga utamaduni endelevu wa kupinga ujangili.

0 comments: