Kapingaz Blog

Monday, January 16, 2017

Mkuu wa Kanisa la KKKT Aonya Upungufu wa Chakula Nchini...........Lowassa, CHADEMA Waahidi Kugawa Chakula Kwa WananchiMkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo ameiomba Serikali kufanya tathmini ya haraka kubaini upungufu wa chakula nchini uliosababishwa na ukame wa muda mrefu. 

Akizungumza wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Meru, Elias Nassari katika Usharika wa Usa River, Wilaya ya Arumeru alisema kuwa Serikali haitakiwi kungoja hadi watu wafe ndiyo waanze kutafuta chakula. 

Dk Shoo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Tarcisius Ngalalekumtwa kuwaandikia maaskofu wote wa kanisa hilo kuwataka waumini wao wafanye maombi, hija, mfungo kwa lengo la kukabiliana na ukame unaolikabili taifa. 

Vilevile, hivi karibuni Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) lilitoa wito kama huo kwa waumini wake, huku Serikali ikisisitiza kuwa hakuna njaa nchini na kuwa haitatoa chakula cha msaada. 

Askofu Shoo aliitaka Serikali iwajibike kufanya tathimini za haraka ili kubaini watu walioathirika na njaa pamoja na kujua idadi kamili ya familia pamoja na kaya zitakazoathirika na njaa ili kupata kiwango sahihi cha misaada ya chakula kitakachoitajika nchini.
 
Habari kwa kina bofya:  HAPA

0 comments: