Kapingaz Blog

Thursday, January 12, 2017

MVUA YAZUA BALAA SHINYANGA, NYUMBA ZAIDI YA 20 ZAEZULIWA NA UPEPO MKALI .


Nyumba zaidi ya 20 zimeezuliwa na upepo mkali wakati mvua ikinyesha usiku huu wa Januari 11,2017 katika manispaa ya Shinyanga.(Habari na RUVUMATV)

Hadi sasa bado haijafahamika kama kuna vifo ingawa mamlaka husika haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo, mvua hiyo iliambatana na upepo mkali pia imejeruhi watu kadhaa katika kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa kata ya Ngokolo kupitia chama cha Demoklasia na Maendeleo(CHADEMA) Emmanuel Ntobi akipewa maelezo na mmoja wa wahanga ambaye amejeruhiwa na paa la nyumba.

Diwani wa kata ya Ngokolo kupitia chama cha Demoklasia na Maendeleo(CHADEMA) Emmanuel Ntobi amefika katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na kujionea uharibifu uliojitokeza kufuatia mvua hiyo


Habari kwa kina bofya: HAPA

0 comments: