Kapingaz Blog

Thursday, February 2, 2017

Agizo la Rais Magufuli latekelezwa, pikipiki 16 zatolewa matari kwa kupita barabara za mwendokasi


Agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli la kulitaka jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kung’oa matairi vyombo vyote vya moto vitakavyopita katika barabara za mabasi yaendayo haraka limeanza kutekelezwa kwa vitendo ambapo pikipiki kumi na sita zimeng’olewa matairi na wahusika wakitarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 2 Febuari mwaka huu.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema kuwa pikipiki hizo 16 zilizotolewa matairi ni sehemu tu ya nyingi zilizokamatwa huku akisema kuwa mkakati huo ni endelevu ambapo wote watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Dkt Magufuli alitoa maagizo kwa askari kukamata magari na pikipiki zinazotumia barabara za mabasi yaendayo haraka na kisha kuzitoa matairi na madereva hao wafikishwe mahakamani. Rais Magufuli alisema madereva hao wakiuliza matairi yao yalipo, wajibiwe kuwa askari hawajaajiriwa kulinda matairi.

0 comments: