Kapingaz Blog

Monday, February 6, 2017

Ajali Yaua Watu 7 Mkoani Kilimanjaro Wakiwemo Waandishi wa Habari


Watu saba wamekufa na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo Mwika, mkoani Kilimanjaro. 

Akizungumza jana katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea saa 11. 00 jioni ikilihusisha lori, gari dogo na pikipiki. 

Alisema lori hilo lilikuwa linatoka Rombo kwenda Dar es Salaam, likiwa limepakia ndizi.

“Breki za lori zilishindwa kufanya kazi na ndipo lilipoligonga gari dogo aina ya Toyota Surf lililokuwa likipishana nalo,” alisema. 

Alisema kabla ya kuanguka lori hilo pia liligonga pikipiki na taarifa za awali ni kuwa watu saba walikuwa wamepoteza maisha. 

Alipoulizwa kuhusu taarifa za kina kuhusu majeruhi na waliopoteza maisha, alisema, “Tuko eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia majeruhi ili kuwapeleka katika Hospitali ya KCMC.” 

Habari kutoka eneo la tukio zilisema gari dogo lilikuwa mali ya kiongozi wa Chama cha Walimu mkoani humo na lilikuwa limewabeba watu watano, wakiwamo waandishi wa habari. 

0 comments: