Kapingaz Blog

Saturday, February 4, 2017

CCM yaja na staili nyingine kuazimisha miaka yake 40 toka ilipoanzishwa.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama hicho siku ya kesho tarehe 5 mwezi wa pili kitakuwa kikitimiza miaka 40 toka kimezaliwa, kimefanya mabadiliko katika kusherehekea siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii

Polepole amesema toka chama hicho kimeanzishwa kimekuwa ni chama cha wananchama na chama ambacho kinashughulika na masuala ya watu watu pamoja na matatizo yao, hivyo mwaka huu wameamua kusherehekea siku hiyo kwa namna tofauti kwani hawatukuwa na sherehe kama desturi yao bali watasherehekea kwa kushiriki shuguli za kijamii.

"Maadhimisho ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidesturi kama ambavyo yamefanyika hapo mwanzoni hivyo hatutakuwa na sherehe kama ilivyodesturi ya mikutano mikubwa ya hadhara , kwa maana ya uzinduzi na kilele isipokuwa mwaka huu tutafanya shughuli za maadhimisho ya CCM kwa namna kuu mbili, moja ni kwa kushiriki shughuli za kijamii, shughuli ambazo moja kwa moja zinagusa maisha ya watu wetu, jambo la pili ni mikutano ya ndani na hapa wanachama wote wa CCM watashiriki mikutano ya ndani kuanzia mikoa, ngazi ya wilaya, ngazi za majimbo, ngazi za kata na ngazi za matawi kwa kushirikisha mashina yetu kote nchini Tanzania."

Mbali na hilo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa maadhimisho ya miaka 40 ya CCM kwa mwaka huu yatafanyika kwa mwaka mzima huu wa 2017.

Ikumbukwe kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).

0 comments: