Kapingaz Blog

Wednesday, February 8, 2017

JESHI LA WANANCHI YATOLEA UFAFANUZI JUU YA VIONGOZI WA SERIKALI WALIOTEULIWA KUTOKA JESHINI KUHUSU KUVAA SARE ZA JESHI WAKIWA KWENYE MAJUKUMU YAO YA KISERIKALI.


Coat_of_arms_of_Tanzania.svg
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa sare za Jeshi kwa viongozi wanajeshi wanaoteuliwa na kupewa madaraka mbalimbali nje ya Jeshi. Hivi karibuni kumekuwa na mjadala juu ya uhalali wa uvaaji wa sare hizo.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kuwataarifu wananchi kuwa kulingana na kanuni za Majeshi ya Ulinzi juzuu ya kwanza, viongozi hao wanaruhusiwa kisheria kuvaa sare za Jeshi wanapokuwa wakitekeleza majukumu maalum, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi hao waliopo katika maeneo yao.
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

0 comments: