Kapingaz Blog

Thursday, February 9, 2017

KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UWT TAWI LA SHIRIKISHO LA WANAFUNZI VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI, LEO


BN648917
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT, Tawi la Shirikisho la Wanafunzi vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Anastazia Malamsha, wakati wa mazishi ya kiongozi huyo, yaliyofanyika leo katika eneo la  Shimbo, Rombo Mkuu mkoani Kilimanjaro. Anastazia alifariki dunia Jumapili, Feb 5, 2017,  katika ajali ya gari wakati akitoka kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya CCM mkoani huo ambapo pamoja naye viongozi wengiewatatu walifariki pia katika ajali hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoaheshima za mwisho kwa mwili wa Anastazia, kabla ya mazishi hayo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Juma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Anastazia wakati wa mazishi hayo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Shaka Hamdu Shaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Anastazia kabla ya mazishi hayo

0 comments: