Kapingaz Blog

Sunday, February 5, 2017

Profesa Lipumba Akanusha Kuwa 'Kibaraka' wa Serikali


Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekanusha tuhuma za kuwa na ukaribu unaotia shaka kati yake na serikali na kutolea ufafanuzi ishu mbalimbali zinazoashiria ukaribu huo ikiwemo ya kuchepusha ruzuku ya chama.

Mwenyekiti huyo anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kinachodaiwa kuwa ni ukaribu wake na serikali, siyo sahihi kwa kuwa yeye huwa anaalikwa tu kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa ambayo hawezi kukataa mwaliko.

"Kwa mfano ukikaribishwa kwenye shughuli ya serikai, labda Rais anazindua kitu, au sherehe za kitaifa na Rais yupo utakataaje" Amesema Lipumba.

RUZUKU
Suala la ruzuku ya chama hicho kuchepushwa pia ni jambo linalodaiwa kuwa ushahdi wa Prof Lipumba kuwa karibu zaidi na serikali, ambapo amesema ilikuwa ni lazima iwe hivyo kutokana na uamuzi wake kama Mwenyekiti wa chama wa kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Fedha, ambaye ndiye aliyekuwa mtia sahihi katika masuala ya fedha.

Pia sababu nyingine ya kuchepusha fedha za ruzuku amesema ni mahitaji ya chama kwa kuwa kilikuwa kinaingia kwenye uchaguzi hivyo kilihitaji fedha kwa ajili ya shighuli mbalimbali.

" Kuhusu ruzuku, nilikuwa nimetengua uteuzi wa mkurugenzi wa fedha, bwana Bashange, kwahiyo hakuwa tena signatory wetu, kwa nafasi yangu kama mwenyekiti niliona hafai, tukajitahidi kufungua akaunti nyingine lakini haikuwezekana. Ikabidi Naibu Katibu Mkuu ambaye ndiye anayeshika nafasi ya Katibu Mkuu anapokuwa hayupo ofisini, aandike barua ya kuomba ruzuku kwa ajili ya mahitaji tuliyokuwa nayo"Ameeleza Lipumba

Lipumba ameendelea kusema "Tukapeleka taarifa kuomba ruzuku. Kwahiyo Naibu Katibu Mkuu akaandika barua kwenda kwa Msajili kuwa tunaomba ruzuku na ipitie kwenye akaunti nyingine, na hilo likafanyika"

MIKUTANO
Kuhusu yeye kuruhusiwa kufanya ikutano, huku Katibu Mkuu wake akizuiliwa, hususani tukio lililotokea mkoani Mtwara, Lipumba amesema hata yeye alipokwenda Mtwara hakuruhusiwa kufanya kilichokuwa kimempeleka, na badala yake aliishia kufanya mikutano ya ndani, huku akibainisha kuwa kilichomkwamisha Maalim Seif ni kwenda bila kutoa taarifa kwa kiongozi wa wilaya.

"Nimekwenda Mtwara, nilikaribishwa na viiongozi wa wilaya, kazi yangu ilikuwa ni kufungua matawi, lakini polisi wakanizuia kuwa sitakiwi kufanya mikutano ya nje, nikafanya mikutano ya ndani...Lakini Maalim Seif alikwenda bila kumtaarifu kiongozi wa wilaya". Amesema

ULINZI
Lipumba aliyekuwa katika mahojiano na kituo kimoja cha TV, amekanusha taarifa za kupewa ulinzi na serikali na kufafanua tukio la kupigiwa saluti na askari, akisema kuwa siku hiyo hakupigiwa yeye saluti bali diwani wa eneo ambalo yeye alishiriki kufanya usafi.

"Pale Buguruni, tulikuwa katika usafi, na tulikuwa na diwani wa eneo lile, askari walikuwa wakiangalia usalama, na alipotokea diwani wa eneo lile, askari walimpigia yeye kwa kuwa ndiye mkuu wa eneo lile, siyo mimi"

Kitendo kilichodaiwa kuwa ni askari kumpigia saluti Prof Lipumba

Katika hatua nyingine, amesema anaendelea kumtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu halali wa CUF,  huku akimtaka amfuate ili wamalize tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja.

0 comments: