Kapingaz Blog

Sunday, April 9, 2017

Alichosema ROMA Mkatoliki baada ya kuruhusiwa kutoka Polisi

Tangu zilipotoka taarifa kuwa ROMA Mkatoliki na wenzake watatu waliokuwa wamekamatwa na watu wasiojulikana wamepatikana wakiwa wazima Watanzania wengi wamekuwa na shauku ya kujua ni jambo gani kina ROMA wanaweza kuzungumza kuhusu tukio hilo.
Baada ya kuruhusiwa na Polisi, ROMA amezungumza kwa ufupi kuhusu tukio hilo lakini akiwa hayupo tayari kuelezea kwa undani hadi pale watakaporuhusiwa na Polisi kwani kwa sasa taratibu za kiusalama haziwaruhusu kuelezea ni nini kimetokea.
“Kwa kifupi tu niwahakikishe mimi ni mzima niko vema kabisa kiafya, kiakili na vinginevyo na hata wenzangu watatu nikimaanisha Mona, Bin Laden pamoja na Imma, tunaendelea vizuri na kwa sasa tupo katika taratibu za kutoa taarifa ya tukio zima, taratibu hizo zinatufunga tusiongee chochote kwa sasa hivi,
“Ratiba ninayoweza kuwapa kupita kesho jumapili, siku ya jumatatu nadhani kutakuwa na press conference ya kuelezea habari nzima ilikuwaje, nawashukuru Watanzania wote sijapata nafasi ya kuingia katika mitandao lakini nimepata hadithi zote,” amesema ROMA.

0 comments: