Kapingaz Blog

Wednesday, May 24, 2017

MAELEZO YA MBUNGE WA CCM ALIYEKUWA AKIPINGA UAMUZI WA RAIS MAGUFULI KUHUSU MCHANGA WA DHAHABU MSOME LIVE!!


 Image result for dalali kafumu images

Mhe.Dr.Dalaly Kafumu (Mbunge wa Igunga na Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Viwanda na Biashara) ametoa maelezo yafuatayo kuhusu agizo la kuzuia kusafirisha mchanga nje ya nchi;
______________________________________________Suala la kuhakikisha Tanzania inachenjua madini yote hapa nchini; Mhe Rais yuko sawa kwani ni la kisera; Sera ya Madini ya mwaka 2009 (niliyosimamia utengenezaji wake); kifungu 5.11; policy statement no. 3 inasema hivi: (iii) The Government will collaborate with the private sector, regional and international organisations to strategically invest in smelting and refining.

Kwahiyo mchakato wa kuchenjua mchanga hapa nchini ni matakwa ya kisera lakini shida inakuja tu pale ambapo shughuli hii inaanzishwa kwa haraka na dharura kubwa. Hali hiyo inaweza kuleta uhusiano usio sawa na makampuni ya kimataofa na hata nchi makampuni yanakotoka.

Pia maamuzi haya ya haraka yatatupotezea mapato kama wengine walivyosema. Nia njema na nzuri ya Mhe.Rais ni lazima iendelezwe kwa kumshauri tena Mhe.Rais aangalie namna bora zaidi ya kufikia malengo haya mazuri ya Sera ya Madini ya mwaka 2009.

Washauri wa Mhe Rais - wizara yenye dhamana, tafadhali ni wajibu wenu; na jukumu lenu kumsaidia Mhe Rais juu ya hili jambo jema lenye manufa kwa Taifa letu.

0 comments: