Kapingaz Blog

Monday, June 5, 2017

Kikwete Aibuka.....Asema Kuongoza Nchi Ni Mzigo Mzito, Amtia Moyo Rais Magufuli

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kusema suala la kuongoza nchi ni kazi kubwa mno na kusema yeye toka amestaafu kazi hiyo saizi anaweza kulala na usingizi ukaisha vizuri lakini kipindi cha nyuma haikuwa hivyo.

Kikwete amesema hayo jana kwenye Futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi nyumbani kwake Msoga, Pwani na kusema saizi mzigo huo ameubeba Rais Magufuli na kudai huwa anamtia moyo kuwa anapaswa kupambana kwani hata wao wamepitia mambo ambayo yeye anapitia.

"Sasa nimestaafu muda wa kuwasaidieni ninao tofauti na zamani, zamani mambo mengi kubeba mzigo wa kuongoza nchi kazi kubwa sana saizi anahangaika nao Rais Magufuli wakati mwingine nampa moyo tu bwana wewe pambana, wenzako wote ndiyo hivyo hivyo tulipitia humo humo pale unapodhani unatenda jema asubuhi wanakuponda, ndiyo muziki wenyewe lakini mara kuna hili kuna lile saizi mimi nalala usingizi unaisha kabisa kama kuna watu wananisumbua watakuwa ni wajukuu tu" alisema Kikwete

0 comments: