Kapingaz Blog

Sunday, June 25, 2017

Lowassa Aitaka CHADEMA iitishe Kikao cha Kamati Kuu Ili Kujadili Sakata la Viongozi Wake Kukamatwa Mara Kwa Mara

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ametaka viongozi wa chama hicho kuitisha kikao cha Kamati Kuu ili kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya kuwakamata viongozi wa chama hicho vinavyofanywa na wakuu wa mikoa na wilaya.

Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008, alisema hayo juzi wakati wa futari aliyoindaa kwa madiwani na viongozi wa Chadema na wakazi wa Dar es Salaam iliyofanyika Mikocheni.

Mwanasiasa huyo alisema hayo wakati viongozi wa Chadema, akiwamo Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye walizuiwa kutembelea miradi ya maendeleo kwa madai kuwa kabla ya ziara hiyo, Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifanya kikao cha chama katika jengo la Serikali.

Meya huyo alikamatwa kwa amri ya mkuu wa Wilaya ya Ubungo na kukaa mahabusu kwa saa 48.

Habari kwa kina bofya: HAPA

0 comments: