Kapingaz Blog

Tuesday, June 6, 2017

Uamuzi wa ACT Wazalendo kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Tarehe 03 Juni 2017 Chama chetu kilipokea taarifa kuhusu uteuzi Mama Anna Elisha Mghwira, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Uteuzi wa Mwenyekiti wetu umefanywa akiwa nje ya nchi na baada ya kurejea amefanya mazungumzo na viongozi wenzake wa juu wa Chama kuhusu uteuzi wake huo.

Kufuatia uteuzi huu na kwa kuzingatia unyeti na majukumu ya Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Uongozi ya chama itakutana kesho tarehe 07 Juni 2016 kutafakari pamoja na mambo mengine, namna ambavyo Mama Anna Mghwira atatekeleza wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya.

Chama kinatoa wito Kwa wanachama wote kuendelea na utulivu wakati vikao vya Chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hili.

Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma,
ACT Wazalendo.
Imetolewa leo tarehe 06 Juni 2017

0 comments: