Kapingaz Blog

Wednesday, July 5, 2017

Kubenea Apandishwa Mahakamani Kwa Kumshambulia Mbunge wa CCM


Mbunge wa Ubungo kupitia tiketi ya CHADEMA, Saed Kubenea leo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma na kusomewa shtaka la kumshambulia Mbunge mwenzake wa CCM, Juliana Shoza nje ya viwanja vya Bunge.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha,  Wakili wa serikali Beatrice Nsana amedai kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Julai 3 mwaka huu.

Hata hivyo, Mhe. Kubenea ambaye anatetewa na Mawakili watano amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhaman hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena Julai 26 mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokamilika.

0 comments: