Kapingaz Blog

Tuesday, August 1, 2017

BREAKING NEWSS:: TANZIA: ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA SIASA CHA TADEA MZEE JOHN CHIPAKA AMEFARIKI DUNIA LEO.

Image result for John Chipaka TADEA

Marehemu Mzee John Chipaka Enzi za uhai wake.
Image result for John Chipaka TADEA
Aliyekuwa Mwenyekiti wa TADEA (Marehemu) Mhe. John Lifa Chipaka (Kushoto) akijadiliana jambo na  Mwenyekiti wa UPDP, Mhe. Fahami Dovutwa Enzi za uhai wake.

Taarifa zilizo tufikia hivi punde ni kwamba aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani hapa nchini cha TADEA Mzee John Chipaka amefariki dunia jioni hii katika Hospital ya Ibrahim Haji jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo. 

Marehemu Mzee Chipaka aliwahi kuwa Katibu wa ANC wakati wa kudai Uhuru Enzi za mwalimu Nyerere, vilevile aliwahi kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2015 na jina lake kukatwa na Tume ya uchaguzi kwa kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa na Tume hiyo. 

Taarifa Zaidi za utaratibu wa mazishi tutawajulisha baadae baada ya kupata taarifa hiyo kutoka kwa wana familia.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.


0 comments: