Kapingaz Blog

Thursday, August 3, 2017

Jack Wolper Afunguka Maneno Mazito Kuhusu Jini Kabula


Staa  asiyechuja kunako tasnia ya filamu Bongo, Jacquline Wolper a.k.a Mrs Brown, ameweka wazi hisia za kuguswa na matatizo ya msanii mwenzake, Jini Kabula, ambaye anasumbuliwa na tatizo linalodhaniwa kuwa ni uchizi huku hali yake ya kimaisha ikiwa ni mbaya kiasi cha kukosa makazi.

Wolper ameonyesha kuguswa na kuwaomba wasanii wenzake wote kwa pamoja waungane ili wamsaidie  na kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost  picha ya Kabula na kuandika ujumbe ufuatao:

“Kabula wangu natamani niongee mambo mengi sana juu yako lakini natamani hata kukusaidia urudishe akili yako swali ni kwamba nimechelewa? na kama nimewahi je nitafanikiwa kweli?

“Sasa tuzungumzie jambo jamani maana sijui hizi taarifa tunazipata insta naona na langu niliongelee insta wanatasnia wenzangu tunamsaidiaje mwenzetu, nini kimemkuta, je ninayoyasikia ndiyo hayo, na kama ndiyo mbona kuna wataalam wakusema naye na akakaa sawa.

“Basi Watanzania wenzangu naombeni tuchangie maoni yetu hapa na kama ni mtu ambaye huwezi kutoa ushauri hapa basi tuma msg kwa kupitia namba hii 0765 776 776 ili tuweze kumsaidia Kabula jamani.

“Naandika msg hii huku nalia nina moyo mdogo sana usioweza kuvumilia maumivu nakumbuka nimeshawahi kumwambia Kabula we ni mwanamke mzuri sana Bongo muvi lakini natamani kujua tatizo nini, kacheka tu akachukua nguo akaondoka sikupata muda Wakuzungumza naye.

“Sasa nipo safarini kesho au kesho kutwa nikijaaliwa tukutane kwa pamoja. Bongo Muvi tumfuate alipo jamani tujue tunamsaidiaje, nimeona video anaongea sjui nimechanganyikiwa masikini mimi hata nashindwa kuandika jamani”


0 comments: