Kapingaz Blog

Monday, August 7, 2017

Makonda Atengua Amri ya Polisi ya Kuzuia Magari Tinted

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda amesitisha zoezi lililotolewa na Polisi Mkoa wa Dar es salaam la kuondoa vioo vya magari vyenye giza - Tinted lililopangwa kuanza kesho. 

Makonda amesitisha zoezi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vioo vya giza kutoa ulinzi wa gari ili mtu asiweze kuona kilichomo ndani na kuvunja na kuiba pamoja na kutowatendea haki Watanzania wa mikoani wanaokuja na magari yenye vioo Tinted kwani hilo ni katazo la Mkoa wa Dar es salaam pekee.
 
Sababu nyingine ni wakina mama wanaweka vioo vya Tinted kwavile hawataki kuonekana wako peke yao kwani anaweza kuvamiwa na kuporwa mali pamoja na gari lenyewe.

0 comments: