Kapingaz Blog

Wednesday, August 9, 2017

Msimamo wa CLOUDS MEDIA baada ya Makonda Kugomba Kuomba Radhi

Leo  ulifanyika mkutano na Waandishi wa habari ukimuhusisha Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Ruge Mutahaba, RC wa Dar es Salaam  Paul Makonda na Jukwaa la Wahariri kuhusu swala la kufungiwa kwa habari za Mkuu wa mkoa Paul Makonda.

Baada ya mkutano huo na mengine yaliyojadiliwa na kauli zilizotolewa ikiwemo ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kusema hawezi kuomba radhi, Ruge Mutahaba amehojiwa na vyombo vya habari baada tu ya mkutano huo kuisha na kueleza msimamo wa CLOUDS.

“Baada ya jambo la leo msimamo wa CLOUDS MEDIA GROUP ni uleule tuliokua nao toka siku ya jumamosi baada ya kupatanishwa na Mh. Rais, siku ile alivyotupatanisha sisi kama Watanzania hatukua na budi zaidi ya kukubali na kurudi kwenye uhusiano wa kiuweledi.

“Leo tuliitwa kwenye kikao kwa kutegemea labda kungekua kuna kingine cha ziada lakini…………………………” Amesema Ruge

0 comments: