Kapingaz Blog

Monday, August 7, 2017

"Sitaki haya mambo nikae narudia rudia"... Sikiliza jinsi Rais Magufuli alivyomchimba mkwara mzito waziri wa viwanda Charles Mwijage


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana alielezea kutoridhishwa kwake na hatua zinazochuliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji dhidi ya watu waliouziwa viwanda na kisha kuvitelekeza.


"........kwenye hilo ndiyo unanikwaza. Viwanda ambavyo havifanyi kazi vipo tu kwa nini havifutwi ?, Waziri Mwijage unamuogopa nani wakati mimi ndiye niliyekuteua. 

"Nimekuelezea tukiwa ofisini tukiwa kwenye 'cabinet' na hadharani kote hujanisikia, unataka nikuelekeze nikiwa kaburini ?", alisema Rais Magufuli.
 
==>Msikilize hapo chini alivyomchimba mkwara mzito waziri wa viwanda Charles Mwijage


0 comments: